MABINGWA watetezi Simba leo Aprili 21, Uwanja wa Kaitaba wamesepa na pointi tatu bila ukuta wao kuruhusu bao la kufungwa mbele ya Kagera Sugar .
Mchezo huo ambao ni wa mzunguko wa pili, Simba ilikwenda vyumba vya kubadilishia nguo ubao ukisoma Kagera Sugar 0-2 Simba.
Kipindi cha pili timu zote mbili zilipambana kusaka bao huku Kagera Sugar wakipambana kupata ushindi ngoma ikawa ngumu.
Ni Luis Miquissone dakika ya 13 alipachika msumari wa kuongoza kisha Chris Mugalu alipachika msumari wa pili dakika ya 24.
Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru, ubao ulisoma Simba 2-0 Kagera Sugar.
Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 55 ikiwa tofauti ya pointi mbili na watani wa jadi Yanga wenye pointi 57.
Simba imecheza jumla ya mechi 23 huku watani zao wa jadi wakiwa wamecheza jumla ya mechi 26 msimu wa 2020/21.
Kazi na iendelee
ReplyDeleteHakika,hakuna kulala
DeleteShow show simba 100%
ReplyDelete