April 3, 2021


 DIDIER Gomes,  Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wachezaji wake wameonyesha moyo wa upambanaji kusaka ushindi mbele ya AS Vitaya DR Congo. 

Mchezo wa tano Uwanja wa Mkapa,ubao ulisoma Simba 4-1 AS Vita baada ya dakika 90 kukamilika leo Aprili 3.

Mabao ya Simba yalifungwa na Luis Miquissone dk 30, Clatous Chama alitupia mawili dakika ya 45 na 83 na moja lingine lilipachikwa na Rarry Bwalya dakika ha 66.

Bao la kufuta machozi kwa AS Vita lilipachikwa dakika ya 32 ikiwa ni baada ya dakika mbili kupita kwa Simba kushangilia bao lao la kwanza na lilipachikwa na Soze kwa shuti lililomshinda Aishi Manula. 

Ushindi huo unaifanya Simba kutinga hatua ya robo fainali ikiwa na pointi 13 pamoja na Al Ahly ambayo ina pointi 8 kibindoni na mechi ya mwisho itakuwa dhidi ya Al Ahly ugenini na AS Vita watamaliza na Al Merrikh.

Gomes raia wa Ufaransa ameweza kushuhudia kwa mara ya kwanza mabeki wake wakiokota nyavu kwenye lango lao katika hatua ya makundi, Uwanja wa Mkapa kwa kuwa ilicheza mechi tatu bila kufungwa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Gomes amesema:"Wachezaji wanastahili pongezi kwa sababu wamefanya kazi kubwa, furaha yetu ni kuona kwamba tumetinga hatua ya robo fainali mengine yanakuja,".

5 COMMENTS:

  1. Hongera sana Simba kwa ushindi huu ambao hautisahaulika katika tarehe ya mpira wa Africa Ya Mashariki. Juhudi za Moo zimezaa matunda na wakati uleule nawapa pole wale wanaouota ubingwa na eti kuzoa makombe yote.

    ReplyDelete
  2. Waandishi muwe makini taf...para ya pili toka mwisho: "..kwa kuwa ilicheza mechi tatu bila kufungwa". Hatua hii ya makundi kabla ya mechi ya leo na AS Vita, Simba ilikuwa imecheza mechi NNE (sio tatu) bila kufungwa!

    ReplyDelete
  3. kongore simba
    mmerejesha heshima Tanzania

    ReplyDelete
  4. Asante! Simba kwa kututolea aibu ya Jana maana tungefungwa mmmh!

    ReplyDelete
  5. Ina maana Mwakalebela haruhusiwi hata kushangilia ushindi wa Simba? Daaah!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic