April 24, 2021


 HERRY Mzozo, meneja wa beki wa kushoto wa Simba, Mhaomed Hussein amesema kuwa mteja wake bado hajasaini mkataba na timu yake hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes.

Imekuwa ikielezwa kuwa Mohamed ambaye ni nahodha msaidizi amewekwa kwenye rada za mabosi wa Yanga ambao wanahitaji kuongeza nguvu kwenye kikosi chao.

Meneja huyo amesema:"Mohammed hajasaini Simba kwa sasa ila ipo wazi mkataba wake umebakiza miezi miwili hivyo ikiisha hapo tutajua atabaki Simba ama atarudi Kagera Sugar.

"Ni mchezaji mzuri ambaye anafuatiliwa na wengi hivyo nina amini kwamba kipaumbele cha kwanza kwetu sisi ni timu yake ya Simba kisha mengine yatafuata.

"Unajua kwa hatua ambayo Simba imefika na yeye kucheza mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika wengi wamemuona na wanatambua uwezo wake, kuhusu yeye kwenda Yanga, hakuna ofa niliyopokea," amesema.

Kwenye hatua ya makundi,Simba ikitinga hatua ya robo fainali Mohamed amecheza mechi zote sita za ushindani alianza kikosi cha kwanza.

6 COMMENTS:

  1. Mtu unatunga habari halafu unakanusha mwenyewe

    ReplyDelete
  2. Hizo ni mbinu za kutaka kumpandisha dau

    ReplyDelete
  3. Haondoki ngoo, atachokipata huko atskipsta mara mbili kwa Moo

    ReplyDelete
  4. Moo atawaoa nyie

    ReplyDelete
  5. Ila Yanga isitumike kama ngazi ya kutaka mkataba wa tamaa zaidi.Mchezaji kama anastahiki kulipwa vizuri kutokana na ubora wake basi alipwe vizuri na Mohammed khusen ni miongoni mwa wachezaji hao ila simba kwa kiasi kikubwa ndio iliomtengeneza shabalala tunaemuona leo.Binafsi suala la shabalala kwenda Yanga najua ni porojo tu kwa afya ya maendeleo ya mchezaji mwenyewe ingekuwa inaleta maana kutafuta changamoto mpya nje ya nchi kama ataamua kutoendelea kuchezea simba.

    ReplyDelete
  6. Inaeleweka, wachezaji wa TZ, wakiwa wanataka offer kubwa, badala ya ku-bargain na timu yao husika, lazima waaingizie timu upinzani inawataka. Hapo Mohamedi aseme tu dau lake, asisingizie Yanga. Tuanze kujua thamani zetu wachezaji.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic