April 28, 2021


MHANDISI wa Uwanja wa Azam Complex, Victor Ndozero amesema kuwa wameamua kufanya maboresho makubwa ya uwanja huo kwa sasa baada ya mabosi wa timu hiyo kuamua iwe hivyo.

Ndozero amesema:"Wakurugenzi wa Azam FC wameamua kufanya maboresho makubwa ya uwanja (Azam Complex), kwanza mwaka jana tuliamua kuboresha sehemu ya kuchezea (pitch).



"Leo tumeanza utaratibu wa kubadilisha taa, hizi taa ambazo mlikuwa mnaziona zikitumika kwenye mechi za usiku watu wengi walikuwa wanalalamika mbona kama hatuoni vizuri, mbona kama hazijakaa sawa tukaona ni vema tubadilishe," amesema.

 Kazi ya kuweka taa mpya za kisasa za LED inaendelea ndani ya Uwanja wa Azam Complex kuanzia leo Jumatano, (Aprili 28).

Zoezi hilo pamoja na lile la kuweka mabango ya kielektroniki ya matangazo (LED Display Parameter Board's) kuzunguka uwanja, litachukua wiki mbili hadi tatu hadi kukamilika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic