April 6, 2021


 JUMA Mwambusi, Kaimu Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga amesema kuwa maandalizi ya vijana wake yapo vizuri jambo ambalo linampa furaha ya kufanya vizuri kwenye mechi zake zijazo.

Kikosi hicho kipo kambini Kigamboni kikiendelea na maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.

Mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara ni dhidi ya KMC ambao unatarajiwa kuchezwa Aprili 10, Uwanja wa Mkapa.

Walipokutana Uwanja wa CCM Kirumba, ubao ulisoma KMC 1-2 Yanga, ilikuwa zama za Cedric Kaze ambaye alichimbishwa Machi 7 kwa kile ambacho kilielezwa kuwa ni mwendo mbovu wa timu hiyo.

Mwambusi amesema:-"Wachezaji wanazidi kuimarika na wapo tayari kwa ajili ya mechi zijazo, hata katika mazoezi wanaonekana kuwa imara jambo ambalo ni jema.

"Kikubwa ambacho ninaamini watafanya ni kuleta utofauti na kupata matokeo kwenye mechi zijazo kwani kila kitu kinakwenda sawa," ,

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza jumla ya mechi 23.

Inafuatiwa na Simba iliyo nafasi ya pili na ina pointi 46 baada ya kucheza jumla ya mechi 20.

4 COMMENTS:

  1. Atalia mtu hapo. Huu utakuwa mwanzo mpya baada ya kukosa kwa miaka mitatu. Hatuwachi kitu na fulaha ipo mbele

    ReplyDelete
  2. Mpambane kwa vitendo sio kwa maneno

    ReplyDelete
  3. Mechi za kirafiki. Acheni maneno mengi....

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic