April 27, 2021

 


KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu,  Nassreddine Nabi leo Aprili 27 kimewasili salama Mbeya.

Safari hiyo ni maalumu kwa ajili ya kuwafuata wapinzani wao Tanzania Prisons kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho,  hatua ya 16 bora.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Aprili 30, Uwanja wa Nelson Mandela saa 10:00 jioni.

Yanga ilitinga hatua hiyo baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Ken Gold, Uwanja wa Uhuru.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa wapo imara na wanaamini kwamba watafanya vizuri.


Hesabu kubwa kwa sasa kwa Yanga ni kulitwaa taji hilo ambalo lipo mikononi mwa Simba. 


2 COMMENTS:

  1. Sio kombe hilo tu bali na ubingwa pia

    ReplyDelete
  2. Kamati ya ushindi iko wapi? Mnafikiri kuna Kifukwe walikuwa wanatania?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic