May 2, 2021


 LUC Eymael, raia wa Ubelgiji, kocha wa zamani wa kikosi cha Yanga, amesema kuwa ikiwa timu hiyo itafungwa na Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Mei 8 habari ya kutwaa taji la Ligi Kuu Bara inaweza kuishia hapo.

 

Eymael alifutwa kazi ndani ya Yanga kwa kile kilichoelezwa kuwa ni lugha ya ubaguzi wa rangi jambo ambalo alilipinga.


Eymael ambaye kwa sasa yupo Ubelgiji alisema kuwa anaifuatilia ligi ya Tanzania kwa ukaribu na anatambua kwamba mchezo wa Simba dhidi ya Yanga utatoa picha ya bingwa.

 

“Najua kwamba Yanga watacheza na Simba mchezo wao ujao wa ligi na ikitokea wakifungwa basi safari yao ya kutwaa ubingwa msimu huu itakuwa ngumu kwa kuwa kama Simba watashinda mechi zao ambazo wapo nazo mkononi inakuwa ni fursa kwao kuweza kushinda taji hilo.

 

"Nimeifundisha Yanga na ninajua namna ilivyo, kwangu bado ninahesabu mafanikio makubwa ambayo niliweza kufanya ni kuitoa timu kutoka nafasi ya sita mpaka nafasi ya pili.


"Pia wakati ule niliweza kuifunga Simba kwenye mchezo wa ligi ilikuwa ni baada ya kupita muda wa miaka mitano hivyo Yanga wana kazi ya kufanya," .

5 COMMENTS:

  1. Tutakukumbuka Eymael kwa kuwaongezea utopolo majina mengine mawili, yaani manyani na ma mbwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani alisema wanayanga ni mbwa au nyani?aliwatukana watanzania kama sio waafrika ujue hilo.

      Delete
    2. Huyo uwezo wake wa kufikiri umekomea kwenye alichokiandika

      Delete
  2. Ukubwa wa Simba na yanga utajulikana tarehe 8!!

    ReplyDelete
  3. Manyani au mambwa yatajulikana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic