BODI ya Ligi Kuu Tanzania Bara, (TPLB) kupitia kwa Kamati ya Masaa 72 imemuondoa kwenye ratiba za waamuzi kwenye mizunguko mitatu, mwamuzi msaidizi namba moja Abdulaziz Ally.
Mwamuzi huyo alikuwa kwenye mchezo uliozua utata Uwanja wa Majaliwa baada ya bao alilopachika Yacouba Songne kufutwa licha ya kuonekana lilikuwa ni bao halali na mfungaji alitumia mpira wa kona ya Saido Ntibanzokiza.
Kupitia taarifa rasmi iliyotumwa na TBLB imeeleza kuwa Kamati ya Masaa 72 ilikaa kikao Mei 17 kujadili mwenendo wa matukio mbalimbali ya Ligi Kuu Bara na Ligi Daraja la Kwanza.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Kamati imemudhibu mwamuzi msaidizi namba moja Abdulaziz Ally kwa kumuondoa kwenye ratiba ya waamuzi kwa mizunguko mitatu kwa kosa la kushindwa kumudu mchezo namba 257 baina ya Namungo FC na Yanga.
Pia Meneja wa Klabu ya Gwambina, Mrisho Seleman amefungiwa kwa kipindi cha miezi miwili kutojihusisha na mpira wa miguu na kutozwa faini la laki tatu kwa kosa la kumsumbua mwamuzi wa akiba na kutoa lugha chafu mwamuzi wa kati wakati wakielekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Gwambina Complex Mei 14, ubao ulisoma Gwambina 0-1 JKT Tanzania.
Pia Kocha wa Makipa wa Azam FC, Iddy Abubakar na Mtunza Vifaa wa Azam FC, Yusuph Nzawila pamoja na Edward Msimbe wa Azam FC wamefungiwa kwa kipindi cha miezi miwili kutojihusisha na masuala ya mpira pamoja na faini ya laki tatu kwa kosa la kumtolea maneno makali mwamuzi wa kati.
Ilikuwa ni Mei 15, Uwanja wa Azam Complex wakati ubao ukisoma Azam FC 2-1 KMC.
Kwa upande wa Ligi Daraja la Kwanza, Meneja wa Kitayosce FC, Salum Jumbe amefungiwa kwa kipindi cha miezi miwili kutojihusisha na mpira pamoja na faini ya laki tatu kwa kosa la kutoa lugha chafu kwenye benchi la ufundi ilikuwa ni Mei 07, Pamba 1-0 Kitayosce.
Mbona husemi timu ya yanga imetozwa faini laki tano kwa kosa la kugomea kutumia mpango wa wachezaji badala yake wakatumia mlango wa watazamaji na kusababisha watazaji kadhaa kuingia bure uwanjani?
ReplyDeleteKabla hujawauliza hilo swali ungewauliza kwanza mbona hatujaona wao wenyewe TFF na TPLB wakijipiga faini kwa kuvuruga ratiba ya ligi na kusababisha usumbufu kwa mashabiki
DeleteHata mwamuzi wa kati ana makosa angeadhibiwa pia ili kufuta aibu ya waamuzi wa bongo. Wanatia aibu
ReplyDeleteHaisaidii chochote wangemwacha Sisi tulihitaji lile goli na si vinginevyo
ReplyDeleteNi kweli adhabu ziendelee point tatu walidhurumiwa kirahisi tu kama siyo kibendela hakuwa shabiki wa timu ya upande wa pili
ReplyDelete