May 1, 2021

 


KIKOSI cha Dodoma Jiji kinachonolewa na Kocha Mkuu, Mbwana Makata kimetinga hatua ya robo fainali kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMC.

Mchezo huo ambao umechezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ulikuwa na ushindani kwa timu zote mbili kusaka ushindi.

Wakati KMC ikitupwa nje hatua ya 16 bora na Dodoma Jiji iliokota nyavuni mapema mabao yote kipindi cha kwanza kupitia kwa Seif Karihe dakika ya 19 na Dickson Ambundo dakika ya 41.

Matokeo hayo yanaifanya KMC kuyeyusha ndoto zao za kutwaa taji la Kombe la Shirikisho ili kuweza kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa.

Taji hilo kwa sasa lipo mikononi mwa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes, raia wa Ufaransa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic