May 6, 2021

 


KUELEKA mchezo mkali wa Dabi ya Kariakoo utakaopigwa siku ya Jumamosi, licha ya ubora wa golikipa wa Yanga, Metacha Mnata, lakini unaambiwa rekodi zinambeba zaidi mlinda mlango, Faroukh Shikalo kwa kuliweka salama zaidi lango la Yanga wanapocheza dhidi ya Simba.

 

Ndani ya kikosi cha Yanga, vita ya nafasi ya mlinda mlango ni kali msimu huu, ambapo mara kwa mara Metacha na Shikalo wamekuwa wakipishana na kuzua maswali juu ya nani atailinda milingoti mitatu ya timu hiyo siku ya Jumamosi.

 

Tangu ajiunge na Yanga, Shikalo ambaye ni raia wa Kenya amecheza michezo miwili dhidi ya Simba, ambayo yote iliisha kwa sare ndani ya dakika 90.


Mchezo wa kwanza ambao Shikalo alicheza ni ule wa mzunguko wa kwanza msimu wa 2019/20, ambao iliisha kwa sare ya mabao 2-2 Januari 4, mwaka jana, kabla ya kufanikiwa kuiongoza tena Yanga kwa mafanikio mbele ya Simba kwenye fainali ya Kombe la Mapinduzi Januari 13, mwaka huu.

 

Ambapo mpaka dakika 90 zinakamilika mchezo ulikuwa suluhu na Yanga kushinda kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 4-3.


Kwa upande wa Metacha, yeye amesimama langoni dhidi ya Simba katika michezo mitatu, mchezo wa kwanza ulikuwa Machi 8, mwaka jana, ambapo Yanga walishinda bao 1-0, akadaka tena kwenye kipigo cha mabao 4-1 kwenye Kombe la FA, Julai 12 mwaka jana, kabla ya kuipa sare ya bao 1-1 timu yake katika mchezo wa mzunguko wa kwanza msimu huu, uliopigwa Novemba 7, mwaka jana.


Hii inaonyesha kuwa Shikalo ni salama zaidi kila anapovaana na Simba kuliko Metacha Mnata.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic