May 3, 2021


 UONGOZI wa KMC umesema kuwa kwa sasa umeanza maandalizi ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo.

KMC imetoka kutolewa hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho na Dodoma Jiji kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa hesabu zao kwa sasa ni kwenye mechi zao za ligi ili kupata matokeo chanya.

"Tunawekeza  nguvu zetu kwa sasa kwenye maandalizi ya mechi zetu za ligi ambazo zimebaki na kwa sasa tunaanza kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Namungo FC.

"Utakuwa mchezo mgumu kwa kuwa tutakuwa ugenini ila hatuna cha kuhofia kwani tuna kikosi imara na wachezaji wapo vizuri," amesema.

Kwenye msimamo wa ligi KMC ipo nafasi ya 5 ina pointi 40 inakutana na Namungo FC ambayo ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 31.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic