KUFUATIA sakata lake la kudaiwa kufanya utovu wa nudhamu dhidi ya kocha Nasreddine Nabi, nahodha wa kikosi cha Yanga Lamine Moro ameibuka na kufungukia kuwa hausiki na tuhuma hizo.
Lamine wiki iliyopita aliondolewa kikosini kwenye kambi ya Yanga iliyokuwa ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo, kutokana na madai ya utovu wa nidhamu.
Akizungumzia kuhusu sakata hilo, Lamine amesema: “Mimi si mtovu wa nidhamu kama inavyoelezwa, kabla hatujasafiri kwenda Mtwara nilipata majeraja ambayo benchi la ufundi walilifahamu.
“Kocha aliuliza madaktari kwa nini sifanyi mazoezi, akaambiwa kuhusu majeraha yangu, lakini alisisitiza kwamba nilitakiwa kufanya mazoezi, nikamweleza kuhusu hali yangu lakini alionyesha kutoniamini, kiasi cha kupimwa kwa mara nyingine na ikathibitika kuwa nina majeraha, lakini baadaye nilirudishwa Dar."
sasa mbona magazeti yaliandika vingine na leo habari zingine, what is realy going on in Yanga guys
ReplyDeleteWe Mwandishi kuwa na maadili USITUCHANGANYE ,Kumbuka issue ya Tshishimbi,Molinga we Simba hayo unayoandika Ni Usimba tu unakuponza .Yanga inakuhusu Nini zaidi ya Usimba pls stop acha kaandike mambo ya Simba mna Kampeini ,uliandika makala za utovu wa nidhamu na Wachezaji ukawasema hadharani ulivyo mjinga ,kwani Man City kuwa Bingwa iwe sababu ya kila Timu kufukuza Wachezaji eg Liver,Man u,Chelsea and co na unatoka wazi unaandika kwa ujasiri ,acha upumbavu heshimu maadili Unaiongelea Yanga kwa uchungu upi,ndiyo maana Viongozi wengi wapenda Simba uadirifu hawana hata awe Rais,Waziri Mkuu,Waziri ,Mkuu wa Mkoa nk wanatusumbua ,hizo makala andika za Taifa Stars not Yanga pls Salehe Ally wewe Ni Friends of Simba ,ungeandika makala za kwanini Ligi ya Tanzania imechelewa kuisha na uliwahi kuoana wapi Club inakaa mwezi bila kucheza Ligi kisa inacheza michuano ya Kimataifa, ingekuwa hivyo Ligi ya Uingereza isingeisha Leo. Na hiyo offer wangepewa Yanga ungeandika makala ndefuuuuuu.
ReplyDeleteKwani wewe Ni Kiongozi YANGA ?na huyo Mchezaji mmemtumia kwenye matokeo mabovu ya Yanga .Tunajua yote.
ReplyDelete