KAIZER Chiefs wametangaza kusitisha mkataba wa kocha wao, Gavin Hunt mara moja.
Hunt
alijiunga na Amakhosi mnamo Septemba mwaka jana, kwa ajili ya msimu wa 2020/21.
Katika kipindi alichohudumu ndani ya kikosi cha Kaizer msimu huu, Hunt aliisimamia Kaizer katika michezo rasmi 44 ya mashindano yote akishinda michezo 12, sare 17 na kupoteza mara 15.
Uongozi wa Kaizer umetangaza
kuwa kwa sasa timu hiyo kwa muda itakuwa chini ya makocha wasaidizi, Arthur
Zwane na Dillon Sheppard watakaosimamia timu ya wakubwa, mpaka pale kocha mpya
atakapotangazwa.
Afadhari alivyofukuzwa Ana dharau Sana huyo na Ana bahati angeendelea kuwepo tungeomba mechi nao tuwakomeshe
ReplyDelete