IMEELEZWA kuwa beki wa Yanga Lamine Moro ameondolewa kikosini kutokana na utovu wa nidhamu.
Kwa sasa kikosi cha Yanga kipo Lindi kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC unaotarajiwa kuchezwa leo majira ya saa 10:00 jioni.
Alipotafutwa Kaimu Katibu wa Yanga, Haji Mfikirwa ili azungumzie suala hilo alijibu kuwa yupo safarini.
Mtu wa karibu wa Lamine amesema kuwa nyota huyo kwa sasa hayupo sawa ila hajaweka wazi kinachomsumbua.
Ndio maana makocha wa kigeni wanafaa, kwani wao wanajua kusimamia nidhamu, timu isiyo weza kuthibiti nidhamu ya wachezaji wake ndani na nje ya uwanja lazima iyumbe na ifanye vibaya. Makocha wazawa wana somo la kujifunza juu ya uthibiti wa nidhamu ya wachezaji, ukiwa mpole sana au rafiki sana wachezaji watakupanda juu na utashindwa kuwafundisha. Hongera zake kocha wa Yanga kwa kuanza kufungua makucha.
ReplyDeleteWachezaji walipeni haki zenu sio mnawdhulumu mnajificha kwenye nidhamu, kanuni
ReplyDeletePili pili inakuwashia wapi?
DeleteNaomba kujua KANUNI iliyotumika plz
ReplyDeleteSaido Ntibanzokiza alimfokea Mwambusi hadharani na kulazimisha kutoka wakati akionyesha hasira zake za kuanzishwa benchi. Huu ni utovu wa hali ya juu wa nidhamu, tena afadhali umfanyie dharau kocha huko kambini kuliko uwanjani ambapo watu wengi wanashuhudia. Ntibanzokiza aondolewe kambini kama Lamine
ReplyDeleteMsimu ukiisha tu anarudi kwao maana anajiona anajua sana ilhali hata hapa bongo kuna wachezaji wazuri kumzidi yeye
DeleteAlimfokea kipi, tuwekee clip kuonesha hiyo hali ya kufokea.
Delete