LICHA ya uongozi wa kikosi cha Yanga kufunguka kuwa sakata la nidhamu la nahodha wao, Lamine Moro limemalizwa, nahodha huyo ameibuka na kufungukia kila kitu kuhusu ishu hiyo akikana kuhusika na utovu huo wa nidhamu.
Lamine wiki iliyopita aliondolewa kikosini kwenye kambi ya Yanga iliyokuwa ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo, kutokana na madai ya utovu wa nidhamu.
Akizungumzia sakata hilo, Lamine amefunguka kila kitu ambapo amesema: "Si kweli kuwa mimi ni mtovu wa nidhamu kama ambavyo imekuwa ikiongelewa na baadhi ya watu ikiwemo viongozi wa Yanga. Kabla hatujasafiri kwenda Mtwara nilipata majeraja ambayo benchi la ufundi walilifahamu, tulipofika Mtwara sikufanya mazoezi, lakini nilikuwepo pamoja na timu.
“Kocha aliuliza madaktari kwa nini sifanyi mazoezi, akaambiwa kuhusu majeraha yangu, lakini alisisitiza kwamba nilitakiwa kufanya mazoezi, nikamweleza kuhusu hali yangu lakini alionyesha kutoniamini, kiasi cha kupimwa kwa mara nyingine na ikathibitika kuwa nina majeraha.
“Siku ya mwisho ya mfungo wa Ramadhani, sikuamka vizuri hivyo sikwenda mazoezini, na kutokana na hilo meneja wa timu akanieleza kuwa kocha anahitaji kikao cha pamoja, nikakubali na kwenda kuswali kabla ya kikao.
“Niliporudi sikukuta mtu yeyote sehemu ya kikao, nikarudi chumbani kwangu. Saa mbili baadaye, meneja akanipigia kunijulisha kuwa uongozi umesema natakiwa nirudi Dar es Salaam, Sikusema chochote nikaondoka Mtwara lakini nilikutana na Engineer uwanja wa ndege.
“Baadaye nikaona Ofisa Habari, Hassan Bumbuli amechapisha taarifa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram kwamba sina nidhamu, nilipigana na kocha hivyo ameniamuru niondolewe kikosini. Nikampigia simu Engineer na Dr. Msolla mara kadhaa lakini wote hawakupokea simu zangu.
“Hata nilipomtumia ujumbe Dr. Msolla aliusoma, lakini hakunijibu chochote, nikakaa kimya. Hakuna aliyenitafuta mpaka alipofanya hivyo Kaimu Katibu Mkuu aliponipigia Mei 27, kwamba wananihitaji ofisini.”
Kwa upande wa Ofisa habari wa
Yanga, Hassan Bumbuli kuzungumzia suala hilo amesema: “Kwa sasa sitaki
kuzungumza chochote.”
Wachezaji wetu na viongozi wetu. Mbona mnataka kutupa presha?
ReplyDeleteYanga kuna tatizo la kiuongozi huku wachezaji wakiwa na tatizo la nidhamu... Msola angejiondoa tu mapema ukocha na utawala vinatofautiana sio lazima kila kocha au mchezaji awe mtu wa moira.
ReplyDeleteMimi ni Simba damu lakini kwenye ukweli husema wazi. Namfahamu Lamine ni mtu mpole, mwenye heshima sana. Huenda Yanga wanaishu nyingine lakini sio utovu wa nidhamu kwa huyu jamaa.
ReplyDeleteUongozi ujitafakari. Haiwezekani wachezaji wote wawe watovu wa nidhamu. Uongozi ni kipaji siyo kitu cha kulazimisha kwani kuongoza watu siyo lelemama. Haitakiwi ubabe ni busara na maarifa zaidi ykielekeza mawazo yote kwenye malengo ya timu. Tumekuwa na migogoro na wachezaji kwa muda mrefu sasa mwisho hata wachezaji wazuri watakataa Kuja yanga. Tujitafakari vinginevyo tutakuwa wasindikizaji.Daima mbele nyuma mwiko.
ReplyDelete