May 29, 2021


KOCHA mkuu wa klabu ya Simba, Didier Gomes amefunguka kuwa kikosi chake kimejipanga vizuri kuhakikisha kinafika fainali ya kombe la Shirikisho, na kutwaa ubingwa wa kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo.

Gomes Jumatano iliyopita aliiongoza Simba kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo, baada ya kuiondosha Dodoma Jiji katika hatua ya robo fainali kwa kuifunga mabao 3-0 hivyo kutinga nusu fainali.

Katika hatua ya nusu fainali Simba watavaana na klabu ya Azam katika mchezo ambao unatarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Majimaji, Songea kati ya tarehe 24 hadi 28 mwaka huu, ambapo mshindi wa nusu fainali hiyo atakutana na mshindi wa nusu fainali kati ya Yanga na Biashara United.

Akizungumzia malengo yao kocha Gomes amesema: “Najivunia kujitolea kwa wachezaji wangu mpaka kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya kombe la Shirikisho, malengo yetu ni kuhakikisha tunatetea ubingwa huu kwa mara nyingine tena.

“Tunatarajia mchezo mgumu wa nusu fainali dhidi ya Azam, lakini naamini tutaendelea kucheza katika kiwango bora na kushinda nusu fainali na hatimaye kutwaa ubingwa kwenye fainali.”



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic