KAMA unadhani baada ya kuahirishwa kwa mchezo kati ya Simba na Yanga kuliwaumiza mashabiki pekee, basi sahau hilo kwani hata upande wa wapinzani wa Simba kimataifa timu ya Kaizer Chief imeumia pia.
Ikumbukwe kuwa Simba katika mchezo wa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika wamepangwa kucheza na timu hiyo ya nchini Afrika Kusini, mechi ikitarajiwa kuchezwa Jumamosi hii nchini Afrika Kusini kabla ya kurudiana wiki ijayo.
Chanzo cha ndani cha Simba, kililithibitishia Championi Jumatatu kuwa, Kaizer Chiefs walituma mashushushu wao kuja kuichunguza Simba ikicheza dhidi ya Yanga jambo ambalo lilikwama kutokana na mchezo huo kuahirishwa.
“Katika mchezo wetu ambao ulitakiwa ufanyike dhidi ya Yanga, tayari kulikuwa na wawakilishi wa Kaizer Chiefs, yaani maskauti wao ambao walikuja kuichunguza au kuitazama Simba ikicheza dhidi ya Yanga.
“Lakini kwa bahati mbaya mchezo huo haukufanyika, hivyo dhamira yao haikutimia, walikuja watatu ambao walitua hapa nchini Ijumaa iliyopita, siku moja kabla ya mchezo,” kilisema chanzo hicho.
Simba inatarajiwa kucheza na Kaizer Chiefs Jumamosi hii katika Uwanja wa Soccer City nchini Afrika Kusini katika mchezo wa robo fainali ya kwanza.
kwa upande mwingine Yanga kugomea mchezo ni kitu ambacho huenda kimeisaidia Simba. Maana hio ndiyo nafasi Kaizer wangejifunza kuhusu Simba hata kupitia mchezo wao kwenye TV..Pili ukitizama namna na wingi wa rafu Yanga inazocheza kuna uwezekano baadhi ya wachezaji wa Simba wangekuwa majeruhi..Inaweza kuwa haikuwa mbaya..asante kwa kutoa fursa ya kufanya mazoezi ya nguvu, ila pia nafasi ya kuwaepukisha wachezaji na balaa na kuwapumzisha kwa mechi ijayo
ReplyDeleteUpo sahihi kabisa na shukran nyingi sana kwa Utopolo SC
DeletePorojo za wazee wa mirupo
ReplyDeletePorojo za wabongo, yaani Kaiza Kaiza Chief isubirie mechi moja, wakati kuna mechi nyingi za kuangalia,
ReplyDeleteacheni porojo nyie
Ngoja baada ya matokeo mtajua hamjui
ReplyDeleteama kweli utopolo ni mbumbumbu! bado wanadhani ni Simba ile ya mwaka juzi..Hivi hamjui ndiyo ilimaliza on top ya kundi lake lililo na Al Ahly..na ilifungwa mechi moja na Al Ahly.Kuwa na matumaini sawa na yale ya mwaka juzi ni sawa na ndoto!Ni gongowazi ndio wanajua hawajui.
ReplyDeleteMbumbumbu ni wewe na mama yako kuma wewe
DeleteTaratibu ndugu
DeleteTaratibu ndugu
Delete