WAKATI leo Mei 15 kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu Nassredine Nabi kikitarajiwa kumenyana na Namungo FC, atawakosa nyota nane kutokana na matatizo mbalimbali.
Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Majaliwa ikiwa ni wa mzunguko wa pili na ni kipa Ramadhan Kabwili anatarajiwa kuukosa mchezo huu kwa kuwa bado hajawa fiti kwa mechi za ushindani.
Pia mshambuliaji Wazir Junior huenda akaukosa mchezo wa leo kwa kuwa naye hajawa fiti sawa na beki Dickson Job ambaye kuanza kwake kutategemea hali yake ya leo kwa kuwa alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya nyama za misuli.
Haruna Niyonzima kiungo huyu ana matatizo ya kifamilia na hakusafiri na timu. Pia Carlos Carlinhons ambaye ni kiungo, Yassin Mustapha ambaye ni beki pamoja na Abdala Shaibu, 'Ninja' na Mapinduzi Balama hawa wanasumbuliwa na majeraha.
Hivi timu ya Yanga ina matatizo gani?.
ReplyDelete