May 15, 2021

 


KAIZER Chiefs ambao ni wapinzani wa Simba leo katika Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali ya kwanza majira ya saa 1:00 usiku.

Rekodi zinaonyesha kuwa wapinzani hao wa Simba wakiwa Uwanja wa FNB  hawafungiki kwa kuwa katika mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu hawajapoteza mchezo.

Kwa kuwa wapo imara kama ambavyo Simba imekuwa imara Uwanja wa Mkapa basi leo wawakilishi wa Tanzania kimataifa Simba wana kazi ya kufanya kusaka ushindi.

Katika mechi 9 ambazo wamecheza Uwanja wa FNB hawajapoteza mchezo hata mmoja.

Ikiwa imecheza jumla ya mechi 9, wameshinda nne na  wamelazimisha sare 5. Kupitia ukurasa wao wa Instagram wameweka wazi kuwa kwa sasa akili zao ni dhidi ya mchezo wao wa leo.

"Kwa sasa mawazo yetu ni kwenye mchezo wetu wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba, tuko tayari kwa ajili ya mchezo huo," .

2 COMMENTS:

  1. Leo wwanakaa kimoko tu kinatosha.... This is Simba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic