May 3, 2021


 NYOTA wa zamani wa kikosi cha Yanga, Bakari Malima amesema kuwa ikiwa Simba watawadharau wapinzani wao Mei 8 watafungwa na kupoteza pointi tatu mazima.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes itakutana na Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi, Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 1-1 Simba ambapo ni Michael Sarpong alifunga kwa penalti na Joash Onyango naye alitupia bao kwa Simba.

Malima amesema:"Mchezo huo utakuwa mgumu na kila timu inahitaji pointi tatu hivyo wengi wanaipa matumaini Simba lakini mpira una matokeo ya kushangaza.

"Ikiwa Simba wataingia kwa kujiamini kupita kiasi na kusahau kwamba Yanga nao wanahitaji pointi tatu itakuwa rahisi kwao kufungwa na kupoteza pointi tatu.

"Kikubwa kwa timu zote mbili ni kuwa na nidhamu na kucheza kwa kuamini kwamba hata wapinzani wao wanahitaji pointi tatu muhimu," amesema. 

4 COMMENTS:

  1. Labda suluhu Ila sio ushindi,mungu akuweke mpaka mwisho wa ligi.

    ReplyDelete
  2. Kopo tupu Lina kelele nyingi lililojaa husikii kitu ila utasikia tu

    ReplyDelete
  3. Kwa nini asiseme "Ikiwa Yanga wataidharau Simba, watapoteza mechi"?

    ReplyDelete
  4. Mbona mna wasiwasi kwani kila kisemwacho inakusudiwa yanga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic