DOZI ambayo inatolewa kwa sasa na Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes, raia wa Ufaransa kwa wachezaji wake ni hatari kwa kuwa ni bandika bandua, bila kuonyesha tabasamu kwa wachezaji hao.
Picha ipo hivi mara baada ya ubao wa Uwanja wa FNB City Soccer City kusoma Kaizer Chiefs 4-0 Simba, siku ya pili walianza mazoezi nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudio unaotarajiwa kuchezwa Mei 22, Uwanja wa Mkapa.
Kikosi kiliporejea Bongo, Mei 17, wachezaji walipumzika kwa masaa kadhaa kabla ya jana asubuhi kurejea mazoezini kisha mchana kupiga tizi lingine na jioni tena dozi kuendelea.
Hivyo kwa siku wanafanya mazoezi mara tatu ili kuweza kulipa kisasi mechi yao ijayo kwa kuwa malengo yao ni kutinga hatua ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Taarifa kutoka benchi la ufundi zimeliambia Championi Jumatano kuwa:”Hakuna kupumzika kwa sasa ni kazi muda wote, asubuhi, mchana na jioni ni dozi, hakuna muda wa kucheka tena, kazi inaendelea,”.
Habari zinaeleza kuwa program ya asubuhi, mchana na jioni kila program inatumia masaa matatu hivyo wachezaji wanatumia muda wa masaa tisa kuivutia kasi Kaizer Chiefs bila kucheka.
Meneja wa Simba, Patrcik Rweyemamu ameliambia Championi Jumatano kuwa wanajiandaa vema ili kupata matokeo chanya kwenye mchezo wao ujao.
Hivi huwa Kuna mazoezi ya ziada Timu ipo katikati ya msimu,ninyi Waandishi labda ukiniambia wanataka ku deal na issue za technical zilizowagharimu huko sawa Lakini fitness wakizidisha watakuwa wanajiumiza.Hiyo kutwa Mara tatu inawezekena umetunga brother
ReplyDeleteWatakuwa wanatengeneza uchovu Kama ni kweli hii story
ReplyDeleteHilo ndio dozi sio lile la kula mhogo wa kuchoma kw chumvi halafu kwenda kulala. Kama halitifaa hiyo tarehe 22 basi litafanya kazi hapo mechi ya mwisho wa saba atapokabidhiwa Mnyama ubingwa wake na wengine baki kukodowa macho
ReplyDeleteKwani mwanzoni walikuwa wanachekeana hovyo?
ReplyDeleteDozi sio ishu ishu unaitumia ipasavyo?
Ombi langu kwa wachezaji wetu wa Simba ushindi wa goli 5-0 unawezekana lakini lazima wajitoe kufa kupona, acheni mbwembwe za pila biriani, kila mchezaji wa safu ya mbele ya ushambuliaji na hata viungo (7,8,9,10,11) apambane kuingia ndani ya 18 ya Kaizer na hata nje ya 18 na apige mashuti golini kwa Kaizer mara 4 au 5. Kwa wastani huo tunaweza kutegemea kuona majaribio ya maana. Huwezi kupata goli bila kupiga mashuti golini kwa wapinzani wenu. Simba wakiacha kudhar
ReplyDelete