KOCHA Mkuu wa JKT Tanzania, Abdalah Mohamed, 'Bares' amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Mchezo wa leo utakuwa ni wa kisasi kwa JKT Tanzania huku Yanga wakihitaji kulinda rekodi yao kwa sababu walishinda ule wa mzunguko wa kwanza.
Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Yanga 1-0 JKT Tanzania baada ya dakika 90 kukamilika.
Akizungumza na Saleh Jembe, Bares amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa leo ili kupata pointi tatu muhimu.
"Tunatambua kwamba tunacheza na timu imara ambayo inahitaji ushindi hivyo hata sisi pia tunahitaji ushindi mbele ya Yanga.
"Hautakuwa mchezo rahisi kwetu na kwao pia kwani kila timu ina hesabu zake kwa nafasi ambayo tupo na namna ushindani ulivyo mkubwa ni lazima nasi tupambane bila kuchoka, mashabiki wajitokeze kutupa sapoti," amesema.
JKT Tanzania ipo nafasi ya 14 ina pointi 33 inakutana na Yanga iliyo nafasi ya pili na pointi 58.
JKT piga hao mbuzi warudi bwawani wakajipange upya
ReplyDelete