May 2, 2021


 ZIKIWA zimebaki siku tano kabla ya watani wa jadi Simba na Yanga kumenyana Uwanja wa Mkapa, nyota wa kikosi cha Yanga Said Ntibanzokiza amesema kuwa hana wasiwasi kuelekea mchezo huo na anamini kwamba watapata matokeo.

Ntibazonkiza amekuwa ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Nassredine Nabi ambapo kwenye mechi mbili alianza kikosi cha kwanza mbele ya Azam FC mchezo wa ligi na ule mchezo wa pili wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Tanzania Prisons.

Kiungo huyo mshambuliaji raia wa Burundi amekuwa na uwezo mkubwa wa kucheza na mpira na kupiga mipira ya adhabu akisaidiaina na mshikaji wake Carlos Carlinhos.

Nyota huyo amesema:"Sifuatilii mechi za wapinzani wangu hao mimi sijui ila kikubwa ambacho tunaangalia ni mechi zetu na kuona kwamba tunapata matokeo hakuna jambo lingine.

"Kuhusu kucheza mimi sina wasiwasi pale ambapo ninapata nafasi hivyo ni suala la kusubiri na kuona itakuaje," .

Kwenye msimamo Yanga ipo nafasi ya pili ina pointi 57 baada ya kucheza jumla ya mechi 27 inakutana na Simba iliyo nafasi ya kwanza na pointi zake ni 61 imecheza mechi 25.

4 COMMENTS:

  1. NTOBANZO ANAOMBA ASIPANGWE KUEPUSHA AIBU

    ReplyDelete
  2. Hakuna aibu dude,mpira ni mchezo wa wazi na kuna wakati matokeo yake ni tofauti na matarajio ya wengi,kikubwa tusiende na matokeo yetu.

    ReplyDelete
  3. Anayejua anajua tu, kama ingekuwa ni just bahati tu makombe yasingehudhuria Barcelona, Madrid, Man u, Chelsea, Bayern nk.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic