May 2, 2021

 


JOTO la mtanange wa watani wa jadi Simba na Yanga limeanza kushika kasi baada ya mtathimini ubora wa Simba, Culvin Mavhunga kuanza kuwasoma wapinzani wao Yanga kwenye mchezo ambao Yanga ilipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Azam.

 

Simba na Yanga zitakutana Mei 8, ambapo mchezo wa kwanza uliopigwa Novemba 7 mwaka jana, ulimalizika kwa timu hizo kutoa sare ya bao 1-1 bao la Yanga likifungwa na Michael Sarpong huku lile la Simba likifungwa na Joash Onyango.

 

Mahhunga alikuwa sehemu ya walioshuhudia mchezo huo amesema:-“Wamekuwa na mawasiliano hafifu hasa kwenye eneo la kiungo na eneo la ushambuliaji jambo ambalo limesababisha wanafanya makosa mengi ya kiufundi.


“Kwenye eneo la ulinzi wamekuwa bora kwa baadhi ya mechi licha ya kuruhusu mabao ya aina moja kwenye mechi tatu za mwisho ambazo wamecheza.”

 

Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana Mei 8 kwenye dimba la Mkapa jijini Dar, huku Simba wakiwa na mwenendo bora wakifanikiwa kuwashusha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara Yanga ambao wameongoza kwa kipindi kirefu.

 

 Simba walikuwa kileleni na pointi 61 huku Yanga wakifuata na 57 na Azam wakiwa na 54 kibindoni.

3 COMMENTS:

  1. Kama kweli kasema hivi basi hajui kazi yake. Utawekaje hadharani udhaidu na uimara wa mpinzani wako? Si utakuwa unampa nafasi ya kujipanga kukumaliza?

    ReplyDelete
  2. Sidhani kama mwandishi hii habari niyakweli ..noooooo

    ReplyDelete
  3. No comment coz hii no derby usiishi kwa kukariri chochote kinaweza kutokea ngoja tusubiri

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic