May 13, 2021


MTAMBO wa mabao wa kikosi cha Yanga, raia wa Angola, Carlos Carlinhos ataukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Yanga ikiwa imefunga mabao 41 baada ya kucheza mechi 27 amehusika kwenye mabao matano akifunga matatu na kutoa pasi mbili za mabao.

Nyota huyo alipata maumivu kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora Uwanja wa Nelson Mandela dhidi ya Tanzania Prisons.

Mchezo huo dakika 90 zilikamilika kwa Yanga kushinda bao 1-0 lilifungwa na Yacouba Songne kwa pasi ya Saido Ntibanzokiza.

Hakuweza kumaliza dakika 90 Carlinhos baada ya kupata maumivu na nafasi yake ilichukuliwa na Said Juma Makapu.

Kwenye msafara uliokwe pipa jana kuwafuata Namungo FC Mtwara nyota huyo hakuwepo alibaki Dar kwa ajili ya kuendelea na program maalumu.

Hivyo atakuwa pamoja na kiungo mzawa Mapinduzi Balama ambaye huyu yupo nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Mchezo wa ligi kati ya Namungo FC dhidi ya Yanga unatarajiwa kuchezwa Mei 15, Uwanja wa Majaliwa ambapo utakuwa ni mzunguko wa pili, ule wa kwanza ubao ulisoma Yanga 1-1 Namungo FC.

4 COMMENTS:

  1. Kwani mabao mangapi alioyapata na ikiwa yeye no mtambo WA mabao utawaits nini Akina Chama, Konde boy, Kagere, Boko, Mugalu na wengi wengineo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tutawaita mikia fc......Kenge za mwamedi bhana ko unataka tuwasifie wachezaji wenu....mmeshaaminishwa na ngedele mweupe wenu ndo maana kila kitu mnaamini nyie ni bora....Ila kumbukeni msimu huu tz prisons mmepata point 1 ko acheni roporopo

      Delete
  2. Haji manara hajakosea kusema wachambuzi takataka Simba Ni level nyingine Kwa tz

    ReplyDelete
  3. Hawa kauli zao chafu zisizokwisha ndizo zinazowasababishia mikosi isiyokwisha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic