June 10, 2021


 KLABU ya Chelsea inayonolewa na Kocha Mkuu, Thomas Tuchel imepeleka ofa ya pauni milioni 51.5 kwa ajili ya kumpata beki Achraf Hakimi na ipo tayari kutoa nyota wake wawili.

Hakimi aliibuka ndani ya Inter Milan kwa pauni milioni 36 msimu uliopita akitokea Klabu ya Real Madrid na amekuwa kwenye ubora wake chini ya Kocha Mkuu, Antonio Conte.

Inter Milan imewaweka sokoni nyota wake ambapo imeweka wazi kwamba timu ambao itawahitaji inapaswa kutoa mkwanja kamili na sio maneno.

Ripoti zinaeleza kuwa PSG na Chelsea wameweka pauni milioni 51.5 na Inter Milan wao wanahitaji pauni milioni 68.7.

Imeelezwa kuwa Chelsea wao watatoa dau hilo pamoja na wachezaji wawili ambao ni pamoja na Emerson Palmier na Andreas Christensen kwa ajili ya kumpata Hakimi ambaye alitoa mchango wa mabao 17 msimu uliopita ndani ya Serie A.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic