MSHAMBULIAJI wa zamani wa timu ya Taifa ya Irani, Ali Daei
amempongeza mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiamo Ronaldo
kufuatia nyota huyo kufikia rekodi ya mabao 109 katika michezo ya kimataifa.
Ronaldo alifikia rekodi hiyo baada ya kufunga mabao mawili
kwa mikwaju ya penalti katika mchezo wao wa jana dhidi ya Ufaransa.
Daei aliwasilisha pongezi hizo kupitia mtandao wake wa
kijamii wa Instagram ambapo ameandika: “Hongera sana Cristiano ambaye sasa umebakiza
bao moja kuvunja rekodi ya kufunga mabao kwa wanaume kimataifa.
“Ni heshima kubwa kwamba mafanikio haya kwa sasa yatakuwa ya
Ronaldo bingwa mkubwa wa soka, na binadamu anayejali ambaye pia huchochea huwapa
moyo wengine.”
0 COMMENTS:
Post a Comment