BEKI wa Manchester City, Ruben Dias ameweka rekodi ya kuwa beki wa nne katika historia ya Ligi Kuu England kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa ligi.
Mabeki wengine ambao waliwahi kutwaa tuzo hiyo ni Nemanja Vidic, Vincent Kompany na Virgil van Dijk.
Dias alitangazwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu England akimshinda mchezaji mwenzake wa Manchester City, Kelvin de Bruyne na mshambuliaji wa Spurs, Harry Kane.
Pia katika kikosi bora cha msimu huu ndani ya Ligi Kuu England ambapo mabingwa ni City wenyewe walitoa jumla ya wachezaji sita katika kikosi bora.
Pia Pep Guardiola ametajwa kuwa kocha bora wa msimu akitoka ndani ya Manchester City akiwashinda Ole Gunnar Solskjaer, Brendan Rodgers, David Moyes na Marcelo Bielsa.
0 COMMENTS:
Post a Comment