NYOTA wa Borussia Dortmund, Erling Haaland amemtumia ujumbe kinda wa England, Jude Bellingham aliyeweka rekodi katika mchezo wao na Croatia kwa kuwa mchezaji mdogo zadi kwenye michuano ya Euro 2020.
Bellingham aliichezea England kwa mara ya kwanza katika Euro, juzi akiwa na miaka 17 na siku 349 na kuwa ndiye mchezaji mdogo zaidi wa England kufanya hivyo katika michuano ya Euro pamoja na Kombe la Dunia.
Huko nyuma rekodi hiyo ilikuwa inashikiliwa na beki wa Uholanzi, Jetro Willems ambaye alicheza michuano hiyo 2012 alicheza akiwa na miaka 18 na siku 71.
Haaland alimpongeza nyota huyo ambaye wanacheza naye timu moja kwa kucheza mchezo wake wa kwanza na timu yake ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Croatia. Baada ya mchezo Haaland alisema:"Mchezaji wa daraja la juu mwenye kipaji hongera sana unastahili kuwa hapo,",
0 COMMENTS:
Post a Comment