June 6, 2021


 MWENYEKITI wa Chama cha Wachezaji Tanzania (Sputanza), Mussa Kissoky amesema kuwa wanawakaribisha Yanga na Lamine Moro mezani kujadili matatizo yao.

Hii ni baada ya Lamine kutoa malalamiko ya kudaiwa na klabu yake kuwa ana utovu wa nidhamu.

Hivyo uongozi umewaita ili kuweza kujadili suala hilo na kufikia muafaka kwa kuwa mpaka sasa hakuna ambaye ameweza kufika katika dawati lao.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kissoky amesema kuwa: “Mpaka sasa hatujapata malalamiko yoyote kutoka Yanga wala kwa Lamine Moro, ila kama wameshindwa kuzimaliza tofauti zao waje mezani tutawasikiliza.

 

“Nachukizwa sana na baadhi ya klabu wanavyoficha maovu ya wachezaji wanapoonyesha utovu wa nidhamu, hakuna mwana michezo duniani aliyefanikiwa bila kuwa na heshima, waache hiyo tabia ya kuangalia ukubwa au umaarufu wa mchezaji. 

 

"Halafu kuna suala limezuka kwa baadhi ya klabu mchezaji anapodai stahiki zake anaonekana hana nidhamu, naomba viongozi waangalie hili maana ni haki ya mchezaji kupata haki yake," alisema.

4 COMMENTS:

  1. Huwezi ukakaa meza moja na yanga mkaelewana, yanga ni wabishi na wamejenga taswila kuwa muda wote wao wako right na wengine wanawaonea. Subiri uone.

    ReplyDelete
  2. Yanga ifahamu kuwa ni wajibu kuwalipa waaajiriwa wao haki zao kabla ya kukauka jasho lao na wanapodaiwa wasiwaite wakorofi kwasababu kilichowaleta ni kutafuta riziki kwahivo jambo la kwanza walipwe haki zao na hilo hskuna mjadala

    ReplyDelete
    Replies
    1. so mkude nae anadai au tumetumwa wanazengo

      Delete
  3. Hit team ya yanga viongozi waliopo hawataeweka yanga kwenye mafanikio Bali kwenye migogoro mikubwa hivi wanajua nyumba yenye migogoro inayotoka nje wenye kasoro ni wazazi wenyewe hivi yanga wanajua madhara ya kushindwa kwao Ile kesi ya cas na madhara hata wakishinda wanayajua ?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic