June 6, 2021


 WAPENZI wa soka wa Tanzania sasa wameanza kuingia hamasa baada ya wakongwe wa burudani SuperSport kutangaza kuonyesha mubashara mechi zote za mashindano maarufu ya Uefa Euro 2020 kupitia kisimbuzi maarufu cha DStv.

Mkuu wa Masoko wa DStv Tanzania, Ronald Shelukindo, ametangaza habari hizo njema kwa mashabiki wa soka ambapo DStv inauita msimu wa michuano hiyo kama msimu wa ‘Biriani Ulaya’.


Katika kipindi hicho cha Juni 11-Julai 11, 2021, nyasi zitachimbika katika viwanja mbalimbali barani Ulaya ambapo timu za taifa zitakabana koo kuwania ubingwa huo.

 

“DStv ni wababe wa burudani, na ukiongelea soka basi hapa ndiyo penyewe, hivyo Watanzania wote wakae mkao wa kula, wasubiri kushuhudia ‘Pira Biriani Ulaya’ na mitifuano yote wataishuhudia mubashara kupitia DStv ndani ya chaneli zetu pendwa za SuperSport,” alisema Shelukindo.

 

Kama kawaida yake na kwa fahari kubwa, ili kuongeza utamu na burudani kwa Watanzania, DStv itatangaza michuano hiyo kwa lugha adhimu ya Kiswahili.


“Sisi hatuwapimii wateja wetu burudani, tunataka uone, kusikia na kuelewa kila kinachoendelea uwanjani. Hii ndiyo sababu tumeweka utaratibu wa kutangaza michuano hii kwa Kiswahili,” alisema Shelukindo.


Aliongeza kuwa michuano hiyo itaonekana hadi kwenye vifurushi vya chini kikiwemo kile cha DStv Family na pia baadhi ya mechi zitaonyeshwa kwenye kifurushi cha chini kabisa cha DStv Bomba cha Sh 19,900 tu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic