June 6, 2021


 KOCHA Mkuu wa Ruvu Shooting, Charles Mkwasa amesema kitendo cha wachezaji wake Juma Nyoso na mlinda mlango, Abdallah Rashid kupewa kadi nyekundu kimemvurugia mipango.

Timu hiyo imebakiwa na mechi nne mkononi kukamilisha ratiba kwa msimu wa 2020/21 jambo ambalo anaamini kwamba limevuruga hesabu zake.

 

Kocha huyo ambaye amewahi kuifundisha timu ya taifa, Taifa Stars amesema baada ya wachezaji hao kupewa kadi hizo hana namna zaidi ya kuwaamini waliopo na kufanya nao kazi.

 

“Kiukweli tumefanya makosa na tuliadhibiwa na Simba kwani ukiangalia bao la kwanza ni kutokuwa makini na hata bao la pili wachezaji wangu walizubaa na tukafungwa, hivyo tutakwenda kujipanga ili tufanye vyema kwa michezo minne ambayo imebaki.


"Katika mchezo wetu na Simba wachezaji wangu wawili walipata kadi nyekundu na kiukweli lazima niwe wazi kwamba wataniharibia mipango yangu kwenye timu kiujumla kwani ukiangalia Nyoso ni mchezaji mzoefu na hata golikipa wetu naye ndiye alikua namba moja.


" Lakini kwa sasa sina jinsi natakiwa kuwaamini waliopo ili wanifanyie kazi.Tuko katika vita kubwa kulingana na pointi tulizonazo lakini michezo minne yote tuliyonayo tunacheza kwenye uwanja wetu wa nyumbani bila presha.


" Na mimi kama kocha nitachukua tahadhari zote kuhakikisha nainusuru timu yangu na janga la kucheza playoff au kushuka daraja," amesema,


Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, Ruvu Shooting ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 37.

8 COMMENTS:

  1. Wachezaji wawili tu unalialia kiasi hicho

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nyie akikosekana mmoja tu na mlicheza 11 lakini mkapata kipondo sembise kubaki 8?

      Delete
    2. Umekariri brother,mnaweza mcheze pungufu na mpate matokeo,mpira haupo hivyo unavyojua wewe,alafu simba hii sio hiyo uliyoiweka kichwani wewe ndiomana yeyote anafanyiwa sabu na matokeo yanapatkana ingawa bado umekariri,kadi zingeinufaisha timu pinzani kama zingetoka mapema kadi inayotoka kwakuchelewa maranyingi ni uelewa mdogo tu ila refa alipaswa kutoa penati na kadi ya njano as the first card ila ila kama tayari ulishakua na first card lazima yatokee yale kwani nyoso alionekana dhahiri akifanya upumbavu na hata kipa wa ruvu amefanya ujinga kila mtu aliona.hakuna maonevu hata kidogo ila kwasababu yanga wamezoea kujiona kwamba wako sahihi wakati wote haya lazima wayyatafsiri kama maonevu kwa kuvu,ingawa itawasaidia wao kwenye mechi yao.

      Delete
  2. Hayo ni kaandalizi ya kugawa pointi 3 kwa utopolo ili apate kisingizio kuwa hakuwa na wachezaji wake muhimu, mkwasa msanii

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umesema ukweli kabisa na Utopolo hana presha na mechi hiyo itayo pigwa kwenye dimba la Mkapa

      Delete
    2. Naam wake zangu nimewasikia, ntalishughulikia maoni yenu kikamilifu

      Delete
  3. Kwa nini usingesema kuwa kadi nyekundu ilikuwa ni mipango ya kuidhoofisha timu ili ifungwe kirahisi na Simba kwa kuwa na wachezaji pungufu.

    ReplyDelete
  4. Kipa hakukomaa akili nyoso beki hasiyejitambua refa Kama aliyechezesha mechi hiyo Nampa 90% alifata Sheria bila kuangalia aliadhibu kwa kiasi ghani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic