June 5, 2021


 ISHU ya wachezaji wenye utovu wa nidhamu 
kwenye timu ya Yanga inayowahusu Lamine Moro, Michael Sarpong na Metacha Mnata, bado imekuwa ngumu baada ya kubainika kwamba hakuna chochote kilichojadiliwa.


Hivi karibuni, taarifa zilieleza kwamba, uongozi wa Yanga ulikutana na Lamine kujadili ishu ya utovu wa nidhamu, lakini hakuna chochote kilichotolewa baada ya hapo.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka chanzo cha ndani ya Yanga, masuala ya wachezaji wenye utovu wa nidhamu klabuni hapo bado hayajamalizika.


“Kuna wale wachezaji waliokuwa na utovu wa nidhamu, bado masuala yao hayajakamilika,hivyo yatajadiliwa na uongozi kisha majibu yatatoka.


“Mbali na hayo, kocha mkuu ameonekana kutomuhitaji Lamine ndani ya timu,” kilisema chanzo.


Championi Ijumaa, lilimtafuta Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli kuzungumzia ishu hiyo, alisema: “Masuala ya wachezaji waliokuwa na utovu wa nidhamu bado hayajakamilika mpaka uongozi utakapokaa na kujadili.


“Lakini baada ya timu kurudi kambini na kuanza mazoezi rasmi Jumatatu tayari wote wameanza mazoezi pamoja na wenzao.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic