June 6, 2021


MANCHESTER United huenda ikavunja rekodi ya usajili wa nyota wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho msimu huu ili aibuke ndani ya kikosi hicho.

Licha ya janga la Corona kutibua mipango mingi hasa kwenye uchumi kwa timu nyingi ikiwa ni pamoja za zile za Ujerumani mabosi wa Sancho wamegoma kupunguza bei ya mchezaji wao.

Mwaka uliopita United ilihitaji huduma ya mchezaji huyo ikaambiwa kwamba inapaswa kutoa zaidi ya Euro 100 na msimu huu inaelezwa kuwa wameambiwa watoe Euro 108 kupata saini ya mchezaji huyo.

Ikiwa dili hilo litatimia huenda United ikavunja rekodi ya gharama ambayo ilitumia kwa ajili ya kumpata kiungo wao Paul Pogba iliyokuwa ni Euro milioni 89 mwaka 2016 na akiwa  anashikilia rekodi ya mchezaji ghali ndani ya Ligi Kuu England kwa upande wa madili yaliyokamilika ndani ya United.

Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskajer ameweka wazi kwamba anahitaji kupata mshambuliaji na hesabu ni kumpata nyota huyo.

 


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic