June 6, 2021

 


IMEELEZWA kuwa kikosi cha Yanga kinatarajia kumwaga kiasi kisichopungua Sh milioni 100 ili iweze kumsajili tena aliyekuwa mshambuliaji wao, Heritier Makambo.

 

Yanga inatakiwa kulipa kiasi hicho ili iweze kuvunja mkataba wa mwaka mmoja aliobakisha na klabu yake ya Horoya.

 

Makambo tangu asajiliwe na Horoya mwishoni mwa msimu wa mwaka 2018/19 akitokea Yanga, ameshindwa kutamba ndani ya klabu hiyo kiasi cha Horoya kufikiria kumuuza mchezaji huyo katika dirisha hili linalotarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.


Lakini akiwa Yanga, Makambo alikuwa mmoja wa nyota wa Ligi Kuu Bara, akiifungia timu hiyo mabao 17 msimu wa 2018/19 na kumaliza nafasi ya tatu kwenye chati ya wafungaji nyuma ya Meddie Kagere wa Simba na Salim Aiyee wa Mwadui waliofunga mabao 23 na 18.

 

Aliisaidia Yanga kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 86, nyuma ya Simba waliokuwa na pointi 93.

 

Taarifa za kuaminika kutoka katika chanzo chetu cha uhakika kutoka Yanga kimelithibitishia Championi Ijumaa, kuwa ni kweli wapo katika taratibu za kumrejesha mchezaji huyo ndani ya Yanga.


 Tayari wameshawasiliana na Horoya juu ya kumrudisha mchezaji huyo ambapo wameambiwa na uongozi wa klabu hiyo wanatakiwa kulipa kiasi hicho cha pesa ili kumrudisha mshambuliaji huyo ndani ya klabu hiyo.

 

“Tayari tumewasiliana na uongozi wa Horoya juu ya kumrudisha Makambo ndani ya Yanga lakini wamehitaji tuvunje mkataba wa mwaka mmoja uliobaki wa Makambo wenye thamani ya dola 43,000 za Kimarekani ambazo ni sawa na karibu Sh milioni 100 za Kitanzania ndipo tuweze kumpata Makambo.

 

"Tunachoangalia kwa sasa ni namna gani tutaweza kumpata Makambo, uhakika wa kumpata upo kwa kuwa uongozi wa klabu hiyo una mipango ya kumuuza Makambo, hivyo tutafahamu mwishoni itakuwaje,” kilisema chanzo hicho.


Naye Makambo kupitia mtandao wa kijamii aliandika ujumbe unaoonyesha kuwa ni kweli yupo katika mpango wa kurejea ndani ya klabu hiyo ambapo ujumbe huo ulisoma hivi: “Nimepamisi Tanzania, nimeimisi Yanga na mashabiki wa Yanga.”

4 COMMENTS:

  1. Hapo pana kuns mashaka kwani hayo magoli mafanikio yaliyotajwa yalikuwa karibu miaka mitatu iliyopita, jee kuna hakila uwezo waje bado uwezi wake upo palele au inatosha kuwa hapi zamani alikuwa mchwzaji makini?

    ReplyDelete
  2. Matopolo Sasa hivi wahaharakisha kwa mtindo wa liwe litalokuwa wanachokitaka ni kuifunga Simba na ikiwa majuto ni baadae

    ReplyDelete
  3. Kwa staili hiyo Simba back to back 10 season na ajibu wakamchukue maana masoud juma ashawakana huko haitambui yanga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic