KOCHA Msaidizi wa Simba, Selemani Matola, amefunguka kwamba benchi la ufundi wanakoshwa na aina ya pacha ya washambuliaji wao, John Bocco na Chris Mugalu.
Kocha huyo ameongeza kwamba wanafurahishwa na mwenendo wa wawili hao kwa kuwa wamekuwa wanafunga mabao muhimu katika mechi za timu hiyo.
Bocco na Mugalu wamekuwa wakianza kwa pamoja katika mechi nne mfululizo za mashindano yote kuanzia kwenye mechi dhidi ya Kaizer Chiefs, Dodoma Jiji, Namungo FC na Ruvu Shooting.
Matola amesema: “Tulianza na wawili hao katika mechi na Ruvu kwa ajili ya kufunga, na kweli tukafunga mabao muhimu kwa ajili ya timu kisha baadaye tukamtoa mmoja na kuingiza kiungo.
“Lakini siyo hao tu kwa kuwa tuna kikosi kipana tumekuwa na pacha nyingi katika timu, na wakicheza wanakuwa wanacheza vizuri jambo ambalo ni faida kwetu.”
Kwenye msimamo Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 67 ikiwa imecheza jumla ya mechi 27 wapinzani wao wakubwa ni Yanga wao wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 61.
Mechi ya mwisho ambapo walicheza mbele ya Ruvu Shooting wakati ubao ukisoma Ruvu Shooting 0-3 Simba nyota hao walitupia mabao yote hayo ambapo Bocco alifunga mabao mawili na Mugalu alitupia bao moja.
0 COMMENTS:
Post a Comment