KUELEKEA kwenye mchezo wa kesho Juni 26 kati ya Simba dhidi ya Azam FC ambao ni wa Kombe la Shirikisho tambo zimetawala kwa timu zote mbili kutambiana kwamba zitaibuka na ushindi.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majimaji, Songea ikiwa ni hatua ya nusu fainali.
Upande wa Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes ameweka wazi kwamba wanahitaji ushindi kwenye mchezo huo licha ya ugumu ambao wanaamini kwamba watakutana nao mbele ya Azam FC.
"Azam FC ni timu kubwa na ina wachezaji wazuri kwa kuwa tulikutana nao kwenye mchezo wa ligi na walitupa changamoto, lakini kwa kuwa huu ni mchezo mwingine basi tutapambana ili kushinda," amesema.
Kwa upande wa Vivier Bahati, Kocha Msaidizi wa Azam FC ameweka wazi kwamba maandalizi yapo vizuri na wanahitaji ushindi mbele ya Simba.
"Maandalizi yapo vizuri na wachezaji waliopo wanahitaji ushindi, kikubwa ni kuona kwamba tunaweza kutinga hatua ya fainali ili tuweze kutwaa ubingwa," amesema.
Mshindi wa mchezo wa kesho atakutana na mshindi wa mchezo wa leo utakaowakutanisha Biashara United v Yanga, Tabora.
0 COMMENTS:
Post a Comment