June 25, 2021


 UONGOZI wa Biashara United umebainisha kwamba malengo yao ni kushinda mchezo wa leo mbele ya Yanga utakaochezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Mshindi wa mchezo wa leo ambao ni wa hatua ya nusu fainali atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Simba na Azam FC unaotarajiwa kuchezwa kesho, Uwanja wa Majimaji, Songea.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Biashara United, Idrisa Sechombo amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao ambao utakuwa na ushindani mkubwa.

"Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Yanga hasa ukizingatia kwamba tupo ndani ya tano bora kwenye msimamo wa ligi.

"Wapinzani wetu tunawaheshimu kwa kuwa ni timu kubwa ila ambacho tunahitaji ni ushindi hakuna jambo jingine tunalofikiria kwa wakati huu, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti," amesema. 

Biashara United imetinga hatua ya nusu fainali baada ya kupata ushindi kwenye mchezo wao dhidi ya Namungo FC kwenye mchezo wa robo fainali uliochezwa Uwanja wa Karume, Mara.

2 COMMENTS:

  1. Wanajeshi wa mpakani pigeni hao utopolo kamoja tu kanawatosha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic