June 1, 2021


 KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes, leo Juni Mosi, 2021 kimewasili jijini Mwanza kujiandaa na mchezo wa ligi kuu bara dhidi ya Ruvu Shooting.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa siku ya  Juni 3,Alhamisi, 2021 katika Uwanja wa CCM kirumba uliopo jijini Mwanza.

Kikosi kimetua kikiwa na jumla ya wachezaji 21, pamoja na viongozi 12 wa timu hiyo ikiwa ni pamoja na benchi la ufundi.


  Akizungumza baada ya kufika katika Uwanja wa ndege wa Mwanza, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.


"Wachezaji 21 ambao tupo nao na hesabu ni kuona kwamba tunapata ushindi kwenye mchezo wetu ambao utakuwa na ushindani mkubwa," .

 

Kwenye msimamo Simba ipo nafasi ya kwanza ina pointi 64 inakutana na Ruvu Shooting, yenye pointi 37 ikiwa nafasi ya 10.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic