NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya ya michezo na burudani SportPesa wamezindua kampeni maalum kwa ajili ya mechi za mwezi huu.
Promosheni hiyo ilizinduliwa jana katika ofisi zao Masaki, Dar es Salaam ikihusisha makampuni ya mitandao ya simuTigo, Vodacom na Airtel ikiwa na lengo la kuwazawadia wateja hasa katika kipindi hiki cha michezo ya Euro na nyingine zinazoendelea ikiwemo Copa America na VPL.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa SportPesa, Sabrina Msuya alisema katika kipindi hiki wameona wawazawadie wateja wao wote kwa kuzindua promosheni inayoenda kwa jina la ‘Mshiko Deilee’.
“Promosheni hii inaanza rasmi leo na kumalizika mwezi Julai 11, mwaka huu na kutakuwa na washindi wa kila siku ambao watajishindia kiasi cha Shilingi 10,000 kila mmoja kwa watu 30, pia tutatoa Sh 1Mil kila wiki kwa washindi watatu na mwisho wa promosheni tutatoa 15,888,000 kwa mshindi mmoja mwenye bahati.
“Droo zitachezwa kila siku na washindi watatangazwa kupitia kurasa zetu za Instagram na Facebook, kurasa za washirika wetu ambao ni Tigo, Vodacom na Airtel, pamoja na kurasa za timu za Simba na Yanga”
“Ili kushiriki kwenye promosheni hii ni lazima kuweka pesa kwenye akaunti yako ya SportPesa kisha kuanza kucheza ili kuingia kwenye droo na kupata nafasi ya kuibuka mshindi, kwa wateja wapya watatakiwa kujisajili kwanza kisha kufuata mtiririko huohuo.
“Napenda kuwakaribisha watumiaji wa mitandao yote kushiriki kwenye promosheni hii hata wale ambao hawajajisajili na SportPesa ili waweze kushinda zawadi za kila siku, kila wiki na zawadi kubwa kabisa ya zaidiya Sh 15Mil,” alisema Sabrina.
Akizungumza kutoka Tigo, Fabian Felician alisema “Katika msimu huu wa mechi za Euro na zingine zote tumeona ni vizuri kushirikiana na washirika wetu SportPesa ili wateja wetu wa TigoPesa waweze kubashiri kwa urahisi na kupata nafasi ya kujishindia mamilioni ya pesa," .
Kumbuka mteja wa Tigo kupitia huduma ya Tigopesa anaweza kuweka pesa kwenye akaunti ya SportPesa kwa kupiga *150*01# au kupitiaTigoPesa App.
0 COMMENTS:
Post a Comment