June 10, 2021


 TATIZO la nidhamu kwa wachezaji wenye uwezo mkubwa ndani ya uwanja limekuwa ni jambo la kawaida kwa sasa jambo ambalo linapaswa lifanyiwe kazi na wachezaji wenyewe.

Tabia inapojirudia mara kwa mara hasa inapokuwa ni tofauti na utaratibu ambao umewekwa mahali fulani inakuwa ni kero na muda mwingine tatizo kwa wengine.

Haina maana kwamba kwa sasa lazima kila mchezaji mwenye ubora uwanjani anapaswa asiwe na nidhamu hilo sio sawa jambo la msingi kwa mchezaji ni kuwa na nidhamu.

Wimbo mkubwa ambao unaimbwa kwa sasa ni suala la nidhamu ya nyota wa Simba, Jonas Mkude kushindwa kwenda sawa na uongozi wa Simba.

Jambo la msingi ambalo ni muhimu kwa wachezaji kwa sasa kulifanya ni kuongeza umakini na kufanya kazi yao kwa kufuata miiko ambayo ipo.

Imekuwa kawaida kwa wengi kufanya kinyume na matarajio ya wengi kwa sababu wameamua kuishi kwenye mazingira hayo ambayo ni magumu kwa wengine kuyakubali.

Yote kwa yote tunaweza kusema kwamba jambo la msingi ambalo linapaswa kufuatwa na kila mmoja katika kusaka mafanikio ni nidhamu kisha mambo mengine yatafuata.

Kwa hili suala la Mkude ni muhimu kwa wengine kujifunza na kuwa kwenye mwendo mzuri kwa ajili ya maisha yao kwenye suala la michezo pamoja na masuala mengine.

Ikiwa kwa sasa Mkude anaona ni sawa kwa mambo anayofanya kwa wengine yanawachosha basi kesho ikifika atajuta na kutamani kubadili mambo ambayo yametokea nyuma ila itakuwa ngumu.

Kitu pekee ambacho anapaswa kujua kwamba wakati wake ni sasa kuendelea kuishi ndoto zake ila kuwa kwenye migogoro na timu pamoja na wengine kwa tabia zake hilo sio jambo jema.

Ikumbukwe kwamba hivi karibuni alisimamishwa na uongozi wa Simba kutokana na suala la nidhamu na aliahidi kwamba hatarudia makosa ambayo ameyafanya pamoja na makosa mengine mapya ila bado mwendo umekuwa ni uleule.

Labda kuna jambo halipo sawa kwake ni lazima apambane kuweka usawa na kurudi kwenye maisha ya kawaida ambayo ni muhimu kuendelea kupambana na kubaki kwenye ubora wake wa muda wote.

  Wengine ambao wanalitazama suala hili kwa wachezaji ni wakati wao kuweza kujifunza kwa makosa ya Mkude na kuendelea kuishi ndoto zao bila kuwa kwenye matatizo.

Kitu pekee ambacho Mkude anapaswa kufanya kwa wakati huu ni kuangalia pale ambapo anakosea bila kusahau wale ambao wanamzunguka ili aweze kujua tatizo lipo wapi mpaka mambo hayo kujirudia mara kwa mara.

Ipo wazi kwamba kila mtu ana jambo lake ambalo anapenda kulifanya lakini pale ambapo linazidi na kuwa kero kwa wengine hiyo ni fujo na lazima idhibitiwe kabla ya kuja na matokeo ya tofauti.

Jambo la msingi kwa haya ambayo yanatokea kwa Mkude basi yawe darasa kwa wengine kujua namna itakayowafaya waishi vema.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic