June 8, 2021

 


MWENYEKITI wa zamani wa Klabu ya Simba, Swedi Mkwabi leo Juni 8 ametinga makau makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania,  (TFF) kuchukua fomu ya kugombea urais  wa TFF.

Mkwabi amekwenda kuchukua fomu hiyo kwa niaba ya mgombea Wallace Karia ambaye yeye ndiye mgombea wa nafasi hiyo.

Karia yupo madarakani kwa sasa katika ngazi ya Urais hivyo anahitaji kutetea nafasi yake kwa wakati mwingine tena.

Zoezi la utoaji fomu limeanza leo ambapo zinatolewa makao makuu ya TFF, Karume na fomu zinapatikana kupitia tovuti ya TFF.

Mwisho wa kuchukua fomu na kurejesha ni saa 10:00 Juni 12 mwaka huu.

8 COMMENTS:

  1. Hii inamaanisha nini? Kwani Karia mwenyewe yuko wapi hadi achukuliwe form?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Inamaanisha upendo

      Delete
    2. Tena alomchukulia ni ALIYEKUWA MWENYEKITI WA KLAB YA SIMBA. MAANA YAKE NINI HAPO, NDO UJUE AMEKUWA ANAWAFANYIA MAZURI NDO MAANA

      Delete
  2. Kwanini means Simba ndo ameenda kumchukulia fom

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ulitaka aende Utopolo au nani ili usihoji

      Delete
  3. Vibaraka tu hawa.....
    Nkwabi...simba
    Ntahilaja...yanga
    Hawa wanajitufanya sote mbumbumbu ili tudhani yanga na simba wanamsapoti mme wao Karia.
    Wenye akili tunajua.

    ReplyDelete
  4. Hahahahhahhahaha ALIYEKUWA MWENYEKITI WA SIMBA TENA?????

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic