June 10, 2021


 NYOTA watatu wa timu ya taifa ya Tanzania bado hawajajiunga na timu hiyo ambayo inaendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Juni 13, Uwanja wa Mkapa majira ya saa 10:00 jioni hivyo kunahatihati nyota hao wakakosekana kwenye mchezo huo.

Nyota hao ni pamoja na David Bryson mali ya Azam FC ambaye anasumbuliwa na majeruhi na nafasi yake imechukuliwa na nyota Yohana Nkomola, mwingine ni Simon Msuva ambaye yupo Morocco.

Pia nahodha Mbwana Samatta bado hajaripoti kambini kwa muda wote ambao kikosi kimeanza maandalizi kwa ajili ya mchezo huo chini ya Kocha Mkuu, Kim Poulsen.

Kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya kambi ya Stars, hatma ya nyota hao ipo mikononi mwa Kocha Mkuu, Poulsen ambaye atajua jambo la kufanya juu ya nyota hao.

Nyota wengine ambao tayari wameripoti kambini na wameanza mazoezi ni pamoja na Dickson Job, Abdul Suleiman, Dickson Kibabage, Feisal Salum, Juma Kaseja, Mzamiru Yassin, John Bocco, Edward Manyama. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic