June 10, 2021


SIMBA wameambiwa kwamba hawana hela ya kumlipa nyota wa kikosi cha Al Ahly, Walter Bwalya ambaye anatajwa kuibukia ndani ya kikosi hicho.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes imepanga kufanya maboresho kwenye upande wa safu ya ushambuliaji huku jina la Bwalya ambaye ni mali ya Al Ahly likitajwa.

Mshambuliaji huyo alikuwa akitajwa kuwaniwa na Simba kwa muda mrefu tangu akikipiga ndani ya Nkana FC  ya Zambia ila ikawa ngumu kwa mabosi hao kumpata akaaibukia El Gouna.

Akiwa ndani ya Al Ahyl ya Misiri ameshindwa kuonyesha makeke ndani ya kikosi hicho jambo ambalo linawafanya mabosi wafikirie kumuuza.

 Kwa mujibu wa wakala wa nyota huyo, Paricha Chikoye amesema kuwa ni kweli mchezaji huyo mabosi wake wanataka kumuuza ila kuibukia ndani ya Simba itakuwa ngumu kutokana na mkwanja.

"Ipo wazi kwamba Al Ahly wanataka kumuuza mteja wangu kutokana na kuona kwamba haendani na mfumo ya timu yao hivyo hamna namna lazima wamuuze.

"Imekuwa tetesi kwamba anahitajika na Simba ila ukweli ni kwamba Simba hawana uwezo wa kumlipa fedha ambazo tunahitaji kutokana na mkataba wa kule Al Ahly.

"Kumpata Bwalya sio jambo jepesi na sisi tunahitaji fedha kubwa na siwezi kukutajia kwa sasa hivyo tusibiri na tuone," amesema.

5 COMMENTS:

  1. Hahahaaa asante muandishi eti Simba hawana hela za kumleta Bwalya, basi uawashauri wale waliokuwa nazo na ikiwa madeni wachezaji wa zamani wameshalipwa wende wao kumchukua

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bwalya ni mchezaji wa kawaida Sana ya nini kumwagia sifa ya Bei kuliko uwezo wake uwanjani.Wao wenyewe Ahly limewakaa kooni suala la kumwagia mipesa kumsajili wa Bwalya.

      Delete
  2. Hivi mjue baadhi ya Watu humu sijui Ni mapunguani?OK hata Kama Mwandishi katunga habari hao unao maanisha wanaingiaje hapo, au unamaanisha Al Ahly wanadaiwa na Wachezaji?Maana hueleweki wewe?

    ReplyDelete
  3. Kunawatu vichwa vyao vimejaa chuki tu, sasa mchezaji anahitajika na Cimba, yeye anakasirika kuhusu Yanga, sijui watu waaina hii wanapata muda wakufikiria maisha Yao?
    Kweli Tz kuna vichwa ta ajabu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic