June 25, 2021


 KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi leo Juni 25 kimeibuka na ushindi wa baoa 1-0 mbele ya Biashara United ya Mara kwenye mchezo wa nusu fainali.

Mchezo wa leo ambao ulikuwa ni wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho uliochezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ulikuwa na ushindani mkubwa.

Ni Yacouba Songne ambaye alipachika bao la ushindi dk 22 akiwa ndani ya 18 kwa pasi ya mshikaji wake Feisal Salum.

Bao hilo lilidumu mpaka dk 90 ambapo Biashara United licha ya jitihada katika kusaka bao ilikuwa ngumu kwao na kuwafanya waishie hatua ya nusu fainali.

Ushindi wa Yanga unawafanya wasubiri nani ambaye watacheza naye hatua ya fainali kati ya Simba ambao ni mabingwa watetezi ama Azam FC ambao watacheza nusu fainali ya pili, kesho Juni 26, Uwanja wa Majimaji.

6 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic