July 4, 2021

 ZAWAD Mauya, kiungo wa Yanga amesema kuwa walikuwa na jamboao ambalo walipanga muda mrefu wanafurahi kuona limetimia.



Nyota huyo jana, Julai 3 aliibuka shujaa baada ya kupachika bao pekee la ushindi mbele ya watani wa jadi, Simba.


Wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 0-1 Yanga, zawadi hiyo kwa mashabiki ilipatikana dk ya 12 kutoka kwa mguu wa Mauya.


Mauya amesema:"Tulikuwa tuna jambo letu ambalo tulipanga tangu awali kulifanya na jambo lenyewe ilikuwa ni ushindi.


"Kwa kilichotokea kwetu ni furaha na tunaamini kwamba mashabiki wamepata kile ambacho walikuwa wanastahili, " amesema.


Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha pointi 70 nafasi ya pili huku Simba ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 73.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic