July 29, 2021

KOCHA msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati amefunguka kuwa watatumia michuano ya kombe la Kagame kujiandaa na michuano ya kimataifa inayotarajia kuanza mwezi Septemba mwaka huu.

Azam FC imethibitisha kushiriki michuano ya kombe la Kagame ambayo inatarajia kuanza kutimua vumbi kuanzia Agosti Mosi hadi Agosti 15 jijini Dar es Salaam ambapo inatarajia kushirikisha timu tisa kutoka mataifa mbalimbali ya ukanda wa CECAFA.

Akizungumzia maandalizi yao kocha Bahati amesema: “Timu tayari imeingia kambini na tunaanza mazoezi kujiandaa na michuano ya Kagame ambayo nina imani itakuwa kipimo tosha kwetu kuelekea michuano ya kimataifa ambayo itaanza hivi karibuni.

”Malengo yetu ni kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa hivyo basi kupitia michuano hii ya kombe la Kagame itakuwa kama sehemu ya maandalizi kuelekea huko ukizingatia tayari tumefanya usajili wa baadhi ya wachezaji ambao nina imani wataingia kwenye mfumo wa timu kupitia michuano hii.”

Azam FC wanaingia kwenye michuano hii wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwenye mchezo wa fainali dhidi ya KCCA mchezo uliopigwa Julai 27, 2019.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic