July 29, 2021

 


MENEJA wa uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Anthony Nyembera amefunguka kuwa tayari maboresho ya uwanja huo yameanza kufanyika, ambapo awamu ya kwanza itahusishwa uwekwaji taa na awamu ya pili itahusishwa uwekwaji nyasi bandia zoezi linalotarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu.

Uwanja wa Jamhuri ni miongoni mwa viwanja vilivyokumbana na sakata la fungia fungia kutoka Bodi ya Ligi kutokana na kutokidhi viwango vilivyowekwa na Bodi, kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara na Ligi Daraja la Kwanza.

Akizungumzia ishu hiyo Nyembera amefunguka:”Kwa sasa tunaendelea na maboresho ya uwanja wetu, na awamu ya kwanza inahusisha uwekwaji taa ambazo zitaruhusu mechi kuchezwa usiku pamoja na shughuli nyinginezo kama matamasha mbalimbali. Awamu ya pili itahusisha uwekaji nyasi bandia zoezi ambalo linatarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu.

“Tunawashukuru ndugu zetu Azam ambao kwa kiasi kikubwa wamechangia maboresho haya hususan kwenye uwekaji wa taa za uwanjani, hivyo wapenzi wa soka jijini Dodoma wakae mkao wa kula mambo mazuri yanakuja.”

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic