IMERIPOTIWA kuwa Klabu ya Chelsea huenda ikamtoa nyota wake Timo Werner kwa ajili ya kumpata Erling Haaland.
Werner aliibuka ndani ya Chelsea msimu uliopita kwa kandarasi ya miaka minne akitokea Klabu ya RB Leipzing kwa dau la pauni 45.5 milioni.
Mambo yake yamekuwa magumu ambapo amefunga jumla ya mabao sita kwenye mechi 35 ambazo amecheza ndani ya kikosi hicho.
Kwa sasa Chelsea inamuwinda Haaland wameamua kumuweka nyota huyo raia wa Ujerumani kama chambo ili kumpata winga huyo wa Dortmund.
0 COMMENTS:
Post a Comment