July 4, 2021


TIMU ya taifa ya England imekata tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali ya Euro 2020 baada ya ubao wa Uwanja wa Olimpico kusoma Ukraine 0-4.

Ushindi huo unaifanya England kuweza kusonga mbele na itapambana na Denmark katika Uwanja wa Wembley katika hatua ya nusu fainali.

Kocha Mkuu wa England, Gareth Southgate alishuhudia mshambuliaji wake Harry Kane akitupia mabao mawili ilikuwa ni dk 4 na 50 huku Harry Maguire akipachika bao moja dk ya 46  na lile la tatu likipachikwa na Jordan Henderson.

Bao la Henderson dk 63 linamfanya awe na furaha kubwa kwa kuwa ni bao lake la kwanza akiwa na timu ya taifa jambo ambalo kwake ni historia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic